Plugins za JOSM

Kifungu hiki kya LearnOSM kipo katika mchakato wa kutafsiriwa. Kama ungependa kusaidia katika kutafsiri tovuti hii, tafadhali tazama CONTRIBUTING.md.

Reviewed 2015-07-14

Jinsi ulivyokuwa mtaalamu katika kutumia mbinu mbalimbali kuhariri, unaweza ukataka kutumia vifaa vingine vya JOSM kuongeza ujuzi wako wa kutengeneza ramani. JOSM inakuwezesha kuweka plugins mbalimbali , ambazo zinaonyesha kazi za zaidi kwa software.

Katika hii sehemu tutajifaunza jinsi ya kuweka plugins, na baadhi ya plugins za muhimu zinazopatikana.

Kuweka Plugins Kuweka Plugins ——————-

  • Muda wowote unaotaka kuweka plugin mpya , nenda Edit > Preferences na bonyeza katika Plugins tab.

Plugins

  • Kama hutaona listi ya plugin zilizopo, bonyeza Download List.
  • Kuweka plugin kiurahisi unaweza kuangalia kisanduku mbele yake na bonyeza OK chini .
  • Mwisho, baadhi ya matoleo ya JOSM inatakiwa urestart JOSM pale unapoweka plugins mpya.

Baadhi ya plugins zinazotumika:

  1. buildings_tools: Kama umechora majengo mengi, hii itafanya kazi iwe rahisi na haraka.

  2. DirectUpload: Kama umekusanya GPS tracks nyingi na ungependa kuzihifadhi katika database ya OSM, hii plugin inafanya iwe rahisi.

  3. editgpx: Kama unataka kuupload GPS tracks kutoka kwenye kifaa cha Garmin, unahitaji hii plugin. OSM haitakubali GPS tracks amabzo zimehifadhiwa katika kifaa cha nje cha kuhifadhi taarifa cha Garmin, lakini hii plugin inaweza kurekebisha mafaili wa ajili ya kuupload.

  4. fieldpapers: Hii plugin inakusaidia kuona scanned Field Papers katika JOSM.

  5. imagery_offset_db: Hii plugin inakusaidia kushirikiana na watengeneza ramani wengine ambao wamekuta picha ya anga imehama kidogo. Hili swala limeelezewa zaidi katika sura inayofuata.

  6. mirrored_download: Kwa hii plugin unaweza kupakua eneo kubwa la taarifa katika OSM kwa ajili ya kuhariri.

  7. print: Weka kifaa cha printi , kama ikitokea unataka kutengeneza eneo kwa haraka, amabalo halihitaji kuonekana zuri sana.

  8. utilsplugin2: Ongeza vifaa vingine na menus ya JOSM kwa watumiaji wazoefu. Hii itaelezewa kiundani katika sura inayofuata