Utangulizi

Taarifa zina nguvu. Kwa taarifa nzuri na uelewa wa kweli, watu na jamii wanaweza kuboresha maisha yao na kufanya maamuzi mazuri ya baadae. Kuna watu wengi na mashirika yanayofanya maamuzi yanayoathiri maisha yetu. Taarifa nzuri zinawezesha mashirika binafsi, serikali na raia kufanya maamuzi mazuri na matumaini ya kuboresha maisha yetu. Ramani ni njia nzuri ya kusambaza habari.

A village in Indonesia

Ramani ni picha ya dunia yetu yenye maelezo lukuki. Inaweza elezea wazo flani vizuri kuliko maneno. Hii kwa upande wetu inaweza kusaidia kujibu maswali muhimu. Ni shule au hospitali gani ipo karibu? Nani aliye karibu na huduma hizo? Wapi umasikini ni tatizo zaidi? Maswali kama haya yanaweza elezewa vizuri kwa kutumia ramani, vilevile ramani zinaweza tusaidia kutafuta ufumbuzi juu ya matatizo hayo.

Kama zoezi, chukua kalamu na karatasi harafu chora ramani ya kijiji au mji wako. Ni vitu gani vya muhimu kuweka katika ramani? Je, tarifa ya muhimu zaidi ni hipi? Tumia dakika chache kutengeneza ramani yako, ukimaliza, fikiria kwanini tarifa ambazo umeweka za muhimu, na nani zinaweza kusaidia.

Example of a hand-drawn map

Kama mji wako ni kama mingine, utakuwa na michoro ya vitu kama barabara, mito au mifereji. Pia unaweza kuweka majengo muhimu kama shule, ofisi, viwanja vya michezo na mipaka. Chochote uchoracho utakuwa na alama kama ya boksi kuonesha jengo na vinginevyo. Ramani yako ni picha ya mambo yaliyoko ardhini au hapo mtaani.

Examples of symbols

Ramani yako inatoa taarifa. Unaweza kutumia ramani kumuelezea mtu mwingine wapi sehemu fulani zinapatikana, mbali na hiyo pia ramani inaonyesha wapi matatizo ya jamii yalipo, pia ramani inasaidia kutafuta njia za kupitia. Lakini ikumbukwe kwamba matumizi ya ramani ina mipaka. Kuna nakala moja ya ramani na jinsi unavyoitengeneza ndivyo inaleta maana kwako, lakini sio kama mtu fulani alivyotengeneza ramani kwa namna yake. Kwa sababu ramani ni ndogo kwenye karatasi, kwa hiyo ni vigumu kupata taarifa kwa wengine. Ndio maana tunatengenezea ramani kwenye kompyuta ili mtu yeyote aweze kupata taarifa zilizo sahihi.

Mapping on Computer

OpenStreetMap ni kifaa cha kutengenezea na kushirikishana taarifa za ramani. Mtu yeyote anaweza kuchangia kwenye OpenStreetMap, na maelfu ya watu wanaongezeka kwenye mradi kila siku. Watumiaji huchora ramani kwenye kompyuta, na sio karatasi, lakini kama tutakavyoona kwenye muongozo huu, kuchora ramani kwenye kompyuta sio tofauti sana na kuchora ramani kwenye karatasi. Tunaendelea kuchora mistari kuwakilisha barabara, viwanja, na vitu vyote, na tunaendelea kuwakilisha shule na hospitali kwa kutumia alama. Kitu cha muhimu ni kwamba OSM huhifadhiwa kwenye mtandao wa intaneti, na mtu yeyote anaweza kuipata muda wowote, na bure.

Digital maps with OpenStreetMap

Tunatarajia kwamba utaona OpenStreetMap ni muhimu na ya kuvutia katika kazi zako. Kwa kufuata muongozo huu, utaweza kwa haraka kutengeneza ramani za kidigitali kwa kutumia OpenStreetMap.