Kujifunza Zaidi

Kama umefika mpaka hapa, hongera! Sasa utakuwa na uelewa mzuri jinsi gani ya kutengeneza ramani kwa OpenStreetMap.Vitu gani vingine OSM inawez kufanya? Jinsi gani unaweza kuunganishwa na wanajamii wanaotengeneza ramani?

Sehemu nyingine ya JifunzeOSM

At the end of the chapter on the iD editor you heard about the differences between iD and JOSM. There is an entire section devoted to JOSM where you will learn all the details necessary to fully benefit from the capabilities this editor has to offer.

Mwisho wa hii sura ya iD editor umesikia kuhusu tofauti kati ya iD na JOSM. Pia kuna sehemu yote imehamishiwa JOSM ambapo utajifunza mambo yote ya msingi ya kukuwezesha kufaidika na uwezo unaopatikana katika hii editor.

Kwahiyo,mabadiliko yote yaliyoongezwa kwenye ramani yanategemea na picha ya anga. Lakini unaweza kukusanya taarifa nyingi ukiwa unatembea au unaendesha gari. Hii sehemu ya mobile mapping inaeleza jisi gani ya kukusanya taarifa tofauti na kifaa cha GPS au kwa kutumia vitu maalum vilivyotengenezwa.Pia inaonyesha njia mbalimbali za OpenStreetMap application kwa simu za mkononi.

OpenStreetMap ni njia ya kushirikiana na tunaimani utakuwa sehemu ya waliochangia. Baadhi ya hizi juhudi ni za kujitolea chini ya Humanitarian OSM Team.Kama unapenda kusaidia HOT katika kazi za majanga kama vile Nepal earthquake tafadhali angalia section on coordination. Inahusika na vifaa kuhakikisha kwamba watu wengi wanaweza kufanya kazi pamoja katika eneo dogo na kwa mpangilio unaofaa. Pia inakuwa na muongozo kwa baadhi ya kazi utakazokuwa unafanya unapoungana na hizi kazi.

Jifunze Zaidi

Kuna taarifa nyingi kuhusu OpenStreetMap zinapatikana katika wiki.openstreetmap.org. Hapa unaweza kutafuta taarifa kuhusu miradi mingine inayoendana na OpenStreetMap, na document na tutorial ambazo zinasaidia kujifunza zaidi kuhusu OSM. Wiki

Listi za Anwani za Barua pepe

Njia bora yakujumuika na jumuiya ya watuamiaji wa OpenStreetMap ni kujiunganisha kwenye listi za anwani za barua pepe. Watu wengi wanajiunga kwa kutumia barua pepe zao kwenye listi hizi za OSM , hivi utakapojiunga na Listi hiyo utaweza kutuma barua pepe zako mbali mbali zenye maswali au michango kuhusu OpenStreetMap kwa kundi hilo.

  • Kujiunga kwenye listi za barua pepe za watumiaji wa OpenStreetMap , fungua ukurasa ufuatao ukiwa kweny mtandao
    lists.openstreetmap.org.

Mailing list

  • Utaona ukurasa hapo juu, tafuta listi ya nchi yako kwa kuperuzi kwa kupanda au kushuka kwenye ukurasa huu. Majina ya listi za nchi husika huwa na mfumo kama “Talk-id”, ambapo neno “id” ni ufupisho wa nchi hiyo , ambapo kwa mfano huo ni listi ya nchi ya Indonesia .

  • Chagua listi unayotaka kujiunga nayo.

  • Jaza taarifa husika kwenye viboksi vifuatavyo:

    • Barua pepe yako
    • Jina lako la kwanza
    • Nenosiri jipya
    • Rudia nenosiri
  • Ukishamaliza bonyeza kitufe SUBSCRIBE, ili kujiunga.

  • Sasa fungua barua pepe yako, kama ulivyofanya ulipojiunga na OpenStreetMap.Kutakua na barua pepe kutoka kwenye Listi za barua pepe ulizochagua ili uthibitishe.

  • Bonya linki utakayoiona, ili kuhakiki na kukubali kuunganisha na Kundi listi hilo la barua pepe za Openstreetmap kwa nchi uliyochagua.

  • Sasa utakuwa mwanachama wa listi hiyo.
  • Sasa ukitaka kutuma barua pepe kwenye listi hiyo, tuma kwa anuani talk-id@openstreetmap.org, ukibadilisha “id” na ufupisho wa nchi husika, pia na wewe utapata barua pepe kutoka kwa wanachama wengine wanaotuma barua pepe kwenye kundi hilo.

Ufupisho.

Hizi ni baadhi ya njia unaoweza kuzitumia kujifunza zaidi na kuendelea kuwa karibu na jumuiya ya OpenStreetMap. Tunatumai utaendelea kudadisi na kujifunza zaidi kuhusu OSM na kuendelea kuchangia mradi huu. Tunakutakia uchoraji mwema wa ramani zako!