Jinsi ya kuanza na OpenStreetMap.org
Katika kipande hiki tutajifunza hatua kwa hatua namna ya kuzungusha
tovuti ya OpenStreetMap, kuangalia ramani, na kufungua akaunti ya
mtumiaji. Baada ya kuwa na jina lako la kutumia na neno lako la siri, utaweza
kuchangia pointi yako ya kwanza kwenye ramani.
Tembelea tovuti ya OpenStreetMap
- Kabla ya kuanza, kuwa na uhakika kompyuta yako imeunganishwa na mtandao wa internet.
(Kama wewe unataka kuisoma hii ukiwa kwenye mtandao, basi lazima uwe umeunganishwa!)
-
Fungua mtandao browser yako. Browsers za kawaida ni Firefox, Chrome, Opera, au Internet
Explorer. Kama ni tayari wazi basi unaweza kuunda tabo mpya
- Kwenye juu ya dirisha, ingiza kiungo kifuatacho www.openstreetmap.org:
www.openstreetmap.org
-
Wakati ukurasa unamaliza kufunguka, unapaswa kuona kitu kama
hiki:
Angalia Ramani
-
Kitu cha msingi unatakiwa kuona ramani. Hamisha ramani kwa kubofya
upande wa kushoto bila kuachia kipanya kuelekea chini, na
vuta kipanya kwa kuzungusha (angalia picha hii chini)
-
Kama unatumia kipanya chenye kizungushio, kuza ramani ndani na nje
kwenye ramani kwa kuzungusha kigurudumu cha katikati. Kama hauna
kipanya kilicho na kigurudumu cha katikati, tumia alama ya jumlisha +
na alama ya kutoa – kwa upande wa kulia kwenye kona ya kompyuta yako
(ona mchoro hapa chini).
-
Kutafuta eneo, bofya kushoto katika sanduku limeandikwa “Search” upande
wa kushoto wa ukurasa (tazama picha ya juu). Andika jina la mji wako
au kijiji na ubonyeze Enter. Window inapaswa kuonekana kwa upande wa
kushoto wa ramani na matokeo ya utafutaji wako. Bonyeza kwenye eneo
ambayo inaonekana kama unataka. Ramani moja kwa moja itahamia eneo
ulichagua.
Tazama Ramani Kwa Namna Mbalimbali
Open StreetMap inajumuisha data mbalimbali za kijiografia kutoka sehemu
mbalimbali za dunia. Japokuwa zote zipo kwenye mbegu moja. Data zinaweza
kutafsiriwa kwa namna tofauti na kuwekwa kwa namna tofauti. Kuona haya,
hebu tazama ramani za aina mbalimbali kutoka kwenye tovuti ya OSM.
-
Bofya kulia kwenye kitufe cha tabaka mkono wa kuria wa ramani.
-
Bofya kwenye machagulio tofauti ya ramani. Thibitisha namna ramani
zinavyoweza kubadilika. Kwa mfano, ramani zinazoonesha njia za usafiri
kwa kutumia mizunguko mbalimbali. Data zote hizi kwa urahisi zaidi
zinajumuishwa kwenye mbegu ya OSM.
Kufungua akaunti ya OpenStreetMap
-
Sasa umeshaona jinsi tovuti inavyoonekana,unaweza kujisajiri kwa
jina lako na nenosiri na kwa mara ya kwanza unaweza kuongeza kitu
kwenye ramani.
-
Katika tovuti ya OpenStreetMap,bonyeza “sign up” (ingia) katika kona
ya juu kulia ya ukurasa.
-
Inapaswa uone ukurasa mpya unaoonekana kama hivi:
-
Kuna visanduku vitano katika ukurasa huu ambapo unatakiwa kuvijaza
ili usajiliwe kwenye akaunti na OSM.
-
Ingiza anwani ya barua pepe yako katika visanduku viwili vya mwanzo.
Unatakiwa uingize barua pepe zinazofanana katika visanduku vyote.
Baadaye, unatakiwa kufungua barua pepe yako kuhahakisha akaunti
yako pamoja na OSM.
-
Katika kisanduku cha tatu,inSiza jina ambalo ungependa kuwa nalo.
Autaweza kuchagua jina ambalo mtu mwingine alishachagua kabla
yako, kwahiyo inatakiwa liwe la kibunifu. Kama unajarib kuingiza
kitu rahisi, kama jina lako la kwanza, inawezekana kwamba mtu
mwingine tayari alishatumia hilo jina.
-
Ingiza neno siri jipya katika kisanduku cha nne na tano. Unatakiwa
kuingiza nenosiri linalofanana katika visanduku vyote. Sio lazima
iwe sawa na nenosiri la barua pepe yako.
-
Unaweza kuandika pembeni jina na nenosiri la OSM. Utalihitaji baadae
kuingia.
-
Baada ya kumaliza visanduku vyote, bonyeza “Sign Up” (jiandikishe)
chini ya ukurasa.
-
Kama kuna tatizo lolote, ujumbe wa makosa utajitokeza. Angalia
kuhakikisha kwamba barua pepe yako inafanana katika visanduku
viwili vya mwanzo na neno siri lako linafanana katika visanduku
viwili vya chini. Kama kisanduku cha tatu kimekuwa chekundu,
inamaanisha kwamba mtu mwingine tayari alishachagua hilo jina na
inatakiwa ujaribu jina lingine.
-
Fungua dirisha tofauti au tabo katika browser ya mtandao wako, na hamisha
katika barua pepe yako. Kawaida maeneo ya barua pepe ni
mail.yahoo.com na www.gmail.com.
-
Ingiza anuani ya barua pepe yako na neno siri lako kufungua barua.
Angalizo hii sio inayofanana na jina na neno siri la OpenStreetMap.
-
Kama kila kitu kimefanikiwa katika usajili wako, unatakiwa uone barua
kutoka OpenStreetMap katika inbox yako. Fungua barua pepe. Inapaswa
kuonekana kama picha hii chini. Bofya kwenye kiungo ambayo inaonekana
hapa chini:
-
Dirisha au tabo mpya itafunguka. Kama kila kitu kilienda sawa,
unatakiwa uwe na akaunti ya OSM.
-
Katika ukurasa wa OpenStreetMap, bonyeza “log in” (ingia) katika kona
ya juu kulia. Ingiza jina na neneo siri la OpenStreetMap na bofya ingia.
Unatakiwa sasa uwe umeingia. Unatakiwa uone jina unalotumia katika kona
ya upande wa kulia wa ukurasa.
Kuongeza pointi yako ya kwanza
-
Sasa ukiwa umeingia kwenye tovuti ya Ramani Huria kwa kutumia jina
lako la utumiaji, unaweza kutumia iD Editor kuongeza point yako ya
kwanza kwenye ramani.
-
Peleka ramani kwenye eneo unalolijua vizuri, kama vile mji wako au eneo la makazi. Wazo zuri ni kuhakikisha nyumba yako (au nyumba ya jirani yako) na kazini kwako kumechorwa na kupewa anwani husika.
Kuza ramani mpaka eneo unalotaka kuongeza pointi kwenye ramani (labda mgahawa au duka ambalo halijachorwa bado)
-
Juu ya ramani mkono wa kushoto, kuna kitufe kinaitwa “Edit” kikiwa na pembe
tatu ndogo pembeni yake. Bonyeza pembetatu ndogo. Utaona orodha ikishuka chini.
-
Bonyeza “Edit with iD (in-browser editor)”.
-
Mhariri wa mtandao, jina lake iD, inapaswa kufungua. Utaonekana kitu kama hiki.
-
Unaweza kuongeza pointi kwenye ramani kwa kubonyeza kifungo aitwaye “Point”
kwa juu ya dirisha. Harafu bonyeza kwenye ramani ambapo ungependa kuongeza
kiwango mpya.
-
Chagua kwenye menyu aina ya mahali/sehemu unayoiongeza kwenye ramani. Kisha jaza
fomu itakayotokea na maelezo ya sehemu husika kama jina na tarifa zingine.
-
Kuhifadhi mabadiliko yako, bonya kitufe kilichoandikwa “Save” juu ya ukurasa.
Kwasababu hii ni hariri yako ya kwanza, unaweza kuichezea iD. Usihifadhi mabadiliko
yako kama hujaahakikisha kuwa ni sahihi.
-
Ukibofya Hifadhi (Save), utatakiwa kutoa maelezo ya hayo mabadiliko. Halafu unaweza
kubonyeza kitufe “Save” tena. Na mabadiliko yako yatahifadhiwa kwenye database ya OSM!
Kutumia iD editor ni njia nzuri kufanya mabadiliko kwenye ramani za OPENSTREETMAP kwa urahisi.
Lakini kwenye sura inayofuata tutajadili kwa kini JOSM kama programmu binafsi inayotoa uwezo
zaidi na mabadiliko mengi pia.kuwa huru kuendelea kutumia ID , ukishapata uzoefu zaidi , unaweza
chagua utumie programu ya JOSM au ukurasa wa ID EDITOR.
Ufupisho
Hongera! Ikiwa kila kitu kimeenda vizuri, sasa una jina la mtumiaji na neno
la siri la OpenStreetMap, unafahamu kuipitia tovuti ya OpenStreetMap,
harafu pia umejifunza kiasi kuchora ramani.
Katika sura inayofuata, tutajifunza kuweka programu ya kutengeneza ramani
za OpenStreetMap ambayo inayitwa JOSM, harafu tujifunze jinsi ya kuchora
ramani za tovuti
Kusonga Mbele
Bonyeza kwenye kiungo kwa ajili ya kusoma zaidi: