|
Muongozo wa HOT Remote ResponseHOT ni jamii ya kimataifa inayofanya kazi kwa misingi ya vyanzo huria na data huria kwa msaada wa kibinadamu na maendeleo ya kiuchumi. Jinsi Remote Response Inavyofanya kaziWahusika wengi wa shughuli za HOT hutoa msaada wakiwa mbali. Baada ya kutokea maafa, wahusika wa HOT hutafuta data zilizopo na picha za anga zilizopo. Washirika huwasiliana kupata ODbL picha zinayoendana. Mara baaada ya picha kupatikana wanajamii huchora, au hufuata yaliyopo kwenye picha (kwa kawaida, mtazamo huwa kwenye vitu vyenye kutambulika ambavyo hutumika kutoa msaada wa kibinadamu, kama barabara, majengo, barabara zilizofungwa, mafuriko nakadhalika) na kuzalisha data na ramani. Wakati huu, taasisi zinazohusika huwasiliana kutambua mahitaji yao. Kuzingatia kiwango cha tatizo, HOT inatoa nyenzo muhimu na uwajibikaji unaunganishwa na timu maalumu au wahusika ambao wanahakikisha kila mtu anafahamu wakati nyenzo mpya zinapopatikana na wapi kutazamisha nguvu. HOT inahamasisha wanajamii wa OSM na kama wapo watendaji wa ndani wakutumia vifaa kama Tasking manager kuunganisha jitihada za uwajibikaji. Mfano, kuhusisha kazi zilizofanywa mbali kama Ivory Coast, Senegal, Philippines, and Democratic Republic of the Congo. Muhundo wa kufanya kazi wa HOTMuhundo wa kazi wa HOT (http://tasks.hotosm.org/) ni wazi chombo imeundwa ili kugawanya kazi za ramani kazi kwenye majukumu madogo madogo ambayo yanaweza kukamilika kabisa kwa uharaka. Inaonyesha maeneo ambayo yanahitaji kuchorewa ramani na maeneo ambayo ya ramani yaliyosahihishwa na wengine. Inahusisha pamoja na majukumu ramani kwa ajili ya kuhamasisha (http://wiki.openstreetmap.org/wiki/HOT_activation) , na kudumu kwa Miradi ya kibinadamu (http://hot.openstreetmap.org/projects). Ili kutumia Meneja muhundo wa HOT yakupasa kujiunga na OpenStreetMap ( OSM ) ukiwa na jina la mtumiaji na neno la siri. Kwa maelekezo zaidi soma dodoso la muhundo wa kazi wa HOT (/en/coordination/tasking-manager/). Vifaa vya kuhaririID - iliyotokana na Mapbox kwa mtumiaaji (www.mapbox.com) kiujumlau hiki kifaa kinachukua ubora wa kwanza katika kuhariri. Unaweza kuzindua hii mwingiliano iD ya mhariri dodoso ili kujua jinsi ya kuitumia (http://ideditor.com/). JOSM- Ni Java programu inatamkwa kama “Jaws-um”, ambayo inahitaji kupakuliwa na watu wanajifunza zaidi. Ingawa inachukua mda kuiweka na kujifunza,inafanya kazi haraka wakati wa kuhariri. Inasisitizwa kutumia kipanya wakati wa kuhariri. Ushauri & Neno la Kukupamoyo
Miongozo MingineHuu muongozo umeandaliwa na kukusanywa kutoka kwenye vitabu mbalimbali vilivyokuwepo na muongozo uliofanyiwa kazi kutoka HOT. Unaweza ukapata miongozo mingine katika tovuti zifuatazo. MafunzoLearnOSM’s Remote Mapping Guide- Moja kati ya miongozo mizuri. MapGive’s Learn To Map tutorial- Inavideos ambazo unaweza ukazisimamisha ili ufuatilie vizuri zaidi. HotQuickStartGuide - Imeandikwa na Peter Richardson (@meetar) mtaalamu wa kujitolea wa HOT Remote Response. Kuhusu HOTHOT Wiki Page- Jifunze zaidi jinsi HOT inavyofanya kazi na habari zake mpya. HotCapacities- Inaelezea kazi za HOT kiundani kutoka kwenye tovuti yao.
|