Kifungu hiki kya LearnOSM kipo katika mchakato wa kutafsiriwa. Kama ungependa kusaidia katika kutafsiri tovuti hii, tafadhali tazama CONTRIBUTING.md.

Mchakato wa Kuhariri na JOSM

Kwenye kipengele kilichotangualia tuliiweka JOSM kwenye komputa na kuanza kuchora alama, mistari na maumbo mbalimbali. Ukaongezea presets kwenye hii michoro ili kuongeza tariifa kuhusu vitu hivyo, mpaka mwisho ukafanikiwa kuchora ramani kwa JOSM.

Hili lilikuwa zoezi zuri, sasa uko tayari kuhariri ramani ya OpenStreetMap.

Kwenye kipengele hiki tutaitazama JOSM kwa kina zaidi nakuona mbinu mbalimbali zakufanya mabadiliko kwenye ramani za OpenStreetMap.

Mzunguko Wa Ubadilishaji Ramani

Kuhariri ramani ya OpenStreetMap ni sawa na kuhariri kwa kutumia iD editor kama tulivyoona hapo awali. Lakini kwa sababu JOSM ni programu ya komputa, inafanya kazi tofauti. Mchakato wakuhariri na kuongeza kwenye OpenStreetMap kwa kutumia JOSM ni kama ifuatavyo:

  1. Pakua data za ramani unayoitaka kutoka OSM
  2. Hariri kwa kutumia picha za satellite, GPS, Field Papers na maelezo mbali mbali kama muongozo
  3. Hifadhi mabadiliko kwenye OpenStreetMap.

Upakuaji wa data kutoka OSM —————————

Hatua ya kwanza yakufanya mabadiliko ni kupakua data/taarifa za eneo la dunia unalotaka kuliboresha. Ukumbuke kuwa inabidi ufanye hivi kila unapotaka kufanya mabadiliko kwenye ramani, kwa sababu ramani inaboreshwa mara kwa mara na watumiaji wengine pia kama wewe.

  • Bonyeza kitufe kwenye “File” upande wa kushoto juu wa JOSM harafu bonyeza “Download from OSM” (“Pakupa kutoka OSM”). Dirisha la upakuaji litafunguka. Au unaweza kupata dirisha hili kwa urahisi kwa kubonyeza kitufe cha chakupakua, kilichoonyeshwa hapa:

JOSM Download Button

  • Dirisha la upakuaji utakapofunguka utaona ramani yenye kiboksi cha rangi ya pinki kilichochorwa juu ya ramani. Kama hauioni ramani bonyeza eneo lililoandikwa “Slippy map”.

JOSM Download Dialog

  • Kiboksi cha pinki kinaonyesha eneo ambalo litapakuliwa kwa ajili ya kuhariri. Unaweza kukuza au kusogeza mpaka kwenye eneo unalolifahamu vizuri, kama mtaa wako au kijiji. Mbinu za kusogeza nakukuza ni kama kwenye ramani ya dirisha la JOSM. Kitufe cha kulia cha kipanya kinakuwezesha kusogeza ramani, na kitairi cha kipanya kinakuwezesha kukuza au kupeleka mabali ramani.
Wakati mwingine kama unatumia laptop inaweza kuwa ngumu
kusogeza nakukuza ramani. Ni rahaisi kutumia JOSM na kipanya.
ila laptop nyingi zakisasa zinarahisisha kazi hii kwa kutumia touchpad.
  • Chora kiboksi kwenye eneo unalotaka kupakua. Kuchora kiboksi kipya bofya kwenye ramani, shikilia kitufe cha kushoto cha kipanya chako, vuta kwenye uso wa ramani ili kuchora kiboksi. Achia kitufe ili kumaliza uchoraji.

  • Ukiridhika na ukubwa na mahali kiboksi kilipo, bonyeza “Download” “(Pakua)” chini ya dirisha. JOSM itapata data ya eneo hilo nakuliwasilisha kwenye JOSM kwa ajili ya uboreshaji.

Kuweka Picha

Kama ulifuatilia jinsi tulivyoongeza point za mwanzo na iD editor, ukumbuke kwamba chini ya ramani kuna picha za anga ambazo zitatusaidia kutambua vitu kwenye ardhi. Hii picha imetokea kwa Microsoft Bing, ambao wametoa picha zao kwa ajili ya watumiaji wa OpenStreetMap kuangalia pale wanapochangia kwenye ramani.

  • Kuweka picha za anga za Bing katika JOSM, bonyeza “Imagery” juu katika orodha ya JOSM na chagua “Bing Sat.”

Kama hujaiona Bing Sat katika orodha ya picha, unatakiwa kuactivate katika JOSM preference. Nenda Edit (badili) -> Preference na bonyeza kwenye alama inayosema “WMS TMS”. Unaweza ukatakiwa kubonyeza chini ya mshale kutafuta

![JOSM Preferences up down][]
![JOSM Preferences WMS TMS][]

Bonyeza “Bing Sat”. Halafu Bonyeza “Activate” (“Amsha”.)

Ziara ya JOSM

Sasa tumeshaipakua taarifa ya OpenStreetMap na kuweka picha za anga za Bing, tuangalie muonekano wa JOSM

JOSM layout

Dirisha kuu tayari umeshalielewa na kulizoea - hii ni dirisha la ramani, na ipo pale ambapo mara nyingi kazi inafanyika. Hapa unaweza kuangalia, kuhariri na kuongeza kwenye data za OpenStreetMap.

Upande wa kulia wa dirisha la ramani kuna mfululizo wa panels, na kila panel ina kazi yake. Kawaida unapoweka JOSM kwa mara ya kwanza panel mbalimbali zinaonekana kama vile tabaka, sifa na uchaguzi. Pale unapochagua pionti, mstari au umbo katika dirisha la ramani, itaonekana katika panel ya uchaguzi. Taarifa kuhusu vitu zitaonekana katika “Properties Panel” na jina la mchoraji wa hicho kitu litaonekana katika “Authors panel”.

Hizi panel zinaaweza kufunguliwa au kufungwa kwa kubonyeza vifungo mbalimbali katika upande wa chini kushoto wa JOSM. Chini ya hivo vifungo upande wa juu kulia kuna vifaa ambavyo vinabadilisha kitu unachotaka kufanya na kipanya. Tayari ushavijua baadhi yake, Select tool (kifaa cha kuchagulia) na Draw tool (kifaa cha kuchorea). Kwa chini ya hivo vifaa ambapo panafanya iwe rahisi kukuza, kuchora umbo, kufuta kitu au kutengeneza mstari ambao unaelekeana na mstari mwingine.

Hariri

Hivyo tunakuwa tumekamilisha hatua moja ya mchakato wa kuhariri - Upakuaji. Yumewaandalia JOSM na picha za satelaiti kama rejea. Hatua ya pili ni kuhariri ramani na kuongeza vitu vipya.

Kulingana na eneo kwamba wewe uliamua kulipakua, unaweza kuwa na data nyingi au chache zilizopo. Lakini ona kwamba ni aina hiyo ya data tulizoona awali - pointi, mistari, na maumbo yanayo wakilisha maeneo halisi ya maisha.

  • Tumia mbinu ambazo tayari ulijifunza kuongeza pointi kwenye ramani ya maeneo ambazo unajua. Kama unaweza kuona makosa yoyote, jaribu kuyarekebisha.

  • Huna haja ya kuwa na uharaka wakati wewe unajifunza. Kama huna uhakika kuhusu kitu ni bora ukiache kama ni kilivyo.

  • Kama unataka kusogeza pointi, mstari, au umbo, tumia Chombo cha kuchagua. Bonyeza kwenye pointi na sogeza mahali husika. Hii inaweza kutumika kurekebisha eneo la vitu ambayvo vimewekwa sehemu ambayo siyo sahihi.

JOSM select tool

  • Tumia chombo cha kuchorea kuchora pointi mpya, mistari, na maumbo. Kuelezea vitu hivi nenda kwenye orodha ya Presets, kama ulivyofanya katika sehemu iliyopita.
Kamwe usihariri ramani nje ya eneo ulilo pakua. Unaweza kuona 
  mazingira mstatili uliyo pakuliwa ina msingi imara, wakati eneo hilo 
  ambalao huja pakuliwa lina mistari ulalo. 

JOSM area downloaded

Hifadhi Mabadiliko

Hatua ya tatu na ya mwisho kukamilisha haririshaji wetu ni kupakia mabadiliko tumefanya kwenye OpenStreetMap. Kuhifadhi mabadiliko ni lazima kuwe kumeunganishwa na mtandao.

  • Bonyeza kitufe kwenye “File” kwenye menu ya juu, harafu bonyeza “Upload Data” (“Pakia kwenye OSM”). Dirisha la upakiaji litafunguka. Au unaweza kupata dirisha hili kwa urahisi kwa kubonyeza kitufe cha chakupakia, kilichoonyeshwa hapa:

JOSM Upload Button

  • Dirisha ambayo inaonekana chini inaonyesha orodha ya vitu ulivyoongeza, ulivyo badilisha au vitu ulivyofuta. Katika sanduku chini unaombwa kutoa maoni kuhusu mabadiliko ambayo umefanya. Andika hapa maelezo ya masahihisho yako.

JOSM Upload Dialog

  • Bonyeza “pakia mabadiliko”.

  • Kama hii ni mara yako ya kwanza kutunza mabadiliko kwenye OpenStreetMap, utaulizwa jina lako unalotumia kwenye OpenStreetMap na neno la siri.
  • Ingiza jina na neno la siri kwenye dirisha inaoonekana. Kama ukiweka alama ya tiki kwenye kisanduku katika dirisha hili, jina na neno la siri lako vitatunzwa hakuna haja ya kuingia tena katika siku zijazo au zingine. Bonyeza “Authenticate” “Kuthibitisha”.

JOSM Authenticate

  • You will need to wait a few seconds for your changes to be uploaded, and then you are done! You have edited the map on OpenStreetMap.
  • Unahitaji kusubiri sekunde chache kwa ajili ya mabadiliko yako kwa kupakiwa, kisha tayari! Umetengeneza ramani kwenye OpenStreetMap.

Wakati wewe unahariri, daima kuwa na uhakika wa kupakia mabadiliko
yako kabla hujafunga JOSM. Hata kama bado unahariri, kwanza pakia
mabadiliko yako, na kisha endelea kwa kupitia mchakato huu tena
kwa baadaye wakati una muda mwingine kuhariri. Hakuna haja ya
kupoteza kazi yako!

Kuona mabadiliko yako kwenye ramani

  • Fungua mtandao wako na kusha nenda tovuti http://openstreetmap.org/
  • Peleka ramani mpaka eneo ambalo uliishia kufanyia uharirishaji.
  • Yakupaswa kuona mabadiliko yako kwenye ramani inayoonekana! Kama hujaona, jaribu kubonyeza CTRL+R kuludia tena ukurasa wa mtandao. Wakati mwingine ramani inashindwa kujiupdate vizuri na inahitaji kuludiwa.
  • Niaje kama huoni mabadiliko yako ? Usijali - inaweza kuchukua dakika chache kwa ajili ya mabadiliko kuonyeshwa kwenye ramani. Pia, angalia nyongeza yako katika JOSM kuhakikisha uliongeza mabadiliko kwa usahihi. Nzuri ni kanuni ya jumla, kama pointi yako ina alama katika JOSM, basi kisha ni ya paswa kuonekana kwenye ramani kuu katika tovuti OpenStreetMap.

Ufupisho

Kwa sasa umeonena jinsi ya kuongeza taarifa kwenye OpenStreetMap, kipi kifuatacho? Naam, kuhariri ni kuzuri, lakini siyo suala tu la kutengeneza ramani. Bila shaka unaitaji pia kujifunza jinsi ya kwenda nje na kukusanya taarifa kuhusu maeneo kwenye ardhi.

Katika sehemu ijayo tutajifunza kuhusu njia mbili ambazo ni - GPS na Field Papers, ambazo hutumiwa kukusanyia taarifa za kijiografia. Taarifa kutoka njia zote mbili zinawekwa kwenye JOSM, na kutumika kwa uhariri wa ramani.